Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa ameongoza na na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula wakielekea kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Myerere jijini Dar es salaam tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kulia) na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, kwa pamoja wakipanda ndege leo Mei 24, 2019 jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea Pretoria, Afrika Kuisni kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, Jumamosi Mei 25, 2019.
(PICHA NA IKULU).