Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 16 Mei, 2019 katika kikao cha kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Mhe. Rais Magufuli amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.

Pamoja na kuwataka kuwa waadilifu na wenye nidhamu kazini, Mhe. Rais Magufuli amewataka kusimamia kwa ukaribu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kusimamia ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali, kusimamia ulinzi na usalama na kusimamia rasimali za umma.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya zinazowezesha mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali kwenda vizuri na amewahakikishia kuwa anawaamini na anatarajia wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki cha leo sote tutakwenda kwa mwelekeo mzuri zaidi, nendeni mkachape kazi, mimi ndiye niliyewaweka kwenye nafasi hizo na ninafuatilia utendaji kazi wa kila mmoja wenu, sitarajii kusikia tena hamuelewani miongoni mwenu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Katika kikao hicho Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili viongozi hao katika maeneo yao ya kazi na ameahidi kwenda kuzishughulikia.
Kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mhe. Homera pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Baada ya kikao hicho, viongozi hao wamekula futari na Mhe. Rais Magufuli aliyoiandaa kwa ajili yao.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
16 Mei, 2019