Poshy, Rammy Mshikaji tu
SIKU chache baada ya kuonekana wakiongozana kama mtu na mpenzi wake katika futari maalum iliyoandaliwa na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, mrembo Jacqueline Obed ‘Poshy  Queen’ amesema kuwa yeye na msanii wa Bongo Muvi, Rammy Gallis wala siyo wapenzi kama wengi wanavyodhani bali ni washikaji tu.

Akichonga na Za Motomoto, Poshy mwenye umbo namba nane alisema kuwa, hata siku hiyo alivyotokea wengi waliongea kuhusu nguo ya kubana aliyovaa lakini kwake anaona ilikuwa sawa tu.

“Wabongo wanapenda sana kuongea jamani. Mimi na Rammy kwanza ni washikaji tu, yeye ni Muislam na mimi Mkristo na pia ile nguo niliyovaa wala haikuwa mbaya,” alisema Poshy