Maafisha wa polisi walioharibu gari la mbunge wa Upinzani Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine wakati alipotiwa nguvuni katika siku ya Jumatatu ya Pasaka watakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya nidhamu ya polisi ya matumizi ya nguvu kupita kiasi, amesema Msemaji wa polisi ya Uganda.

Maafisa wa kikosi cha polisi cha kupambana na ghasia (FFU) walivunja madirisha ya gari la Mbunge huyo wa Kyadondo mashariki kwenye barabara ya Busabala alipokuwa akielekea kwenye eneo la One Love Beach kwa ajili ya tamasha la muziki wake aliloliita Kyarenga Extra ambalo baadae lilizuiwa na maafisa wa usalama.

Moi apigwa faini kwa unyakuzi wa ardhi ya mjane
Mbwa amuokoa mtoto mchanga aliyezikwa hai
Bernard Membe akwepa kuzungumzia urais
Maafisa walimzuwia mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwana siasa, na kupasua moja ya madirisha kabla ya kulipiga gesi ya kutoa machozi ndani na kumvuta nje ya gari.

Polisi walimrudisha hadi kwenye nyumba yake ya Magere, Kasangati katika wilaya ya Wakiso baada ya Inspekta mkuu wa polisi Okoth Ochola kupiga marufuku tamasha lake za muziki. Hivi karibuni, rais Museveni, katika taarifa yake, alilaani tukio hilo akisema kuwa polisi wangepaswa kuliburuza gari la mbunge huyo kokote ambako wangetaka kulipeleka.

" Pia sikubaliani na njia iliyotumiwa na polisi kupasua vioovya gari la Bobi Wine. Wangeburuza gari lake na kulipeleka kokote walikotaka kumpeleka ,"Alisema Bwana Museveni katika taarifa iliyotolewa tarehe 4 Mei, 2019.


Matokeo yake kitengo cha udhibiti wa viwango vya taaluma ya polisi (PSU) kinachunguza video zilizochukuliwa wakati wa tukio hilo ili kuwafikisha polisi mbele ya Mahakama ya Nidhamu ya polisi kujibu tuhuma za kutumia nguvu kupita kiasi.


Matumizi ya nguvu kupita kiasi ni kinyume cha sheria ya polisi nchini Uganda . Iwapo afisa wa polisi atapatikana na hatia hiyo hufutwa kazi au kupewa onyo kali.

Msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, anasema hawawezi kupuuza kauli ya rais kwasababu ndiye Mkuu wa Majeshi. Bwana Enanga anasema polisi watatumia utaratibu wa ndani ya polisi kwa kuzingatia maelezo ya rais na kuchukua uamuzi.

Hii si mara ya kwanza maafisa wa polisi kuharibu gari la mwanasiasa wa upinzani au kutumia nguvu kupita kiasi wakati wanapomkamata mwanasiasa