Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu hivi karibuni, Piere Liquid ametimiza ahadi yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo aliyoitoa tarehe 30 Machi katika harambee ya tokomeza zero.

Katika kampeni hiyo ambayo Piere aliahidi kiasi cha shilingi laki moja, lakini amepeleka madawati wanayozidi thamani ya kiasi alichoahidi kwa kupeleka madawati ishirini.

Baada ya kupokea madawati hayo DC Jokate ameandika kuwa; "Leo nimepokea madawati 20 yenye viwango vya juu kutoka kwa Piere Liquid.

Kwenye Harambee yetu ya tarehe 30/03/2019 aliahidi kutoa laki moja lakini leo amekuja na madawati 20 yenye thamani ya zaidi ya Tsh laki moja. Kwa niaba ya Wanakisarawe nasema asante sana kwa mchango wako bado ahadi ya kutengeneza madawati na hii kampuni inabaki. Asante".

Machi 31, 2019 Piere aliahidiwa na Jokate kupewa tenda ya kutengeneza madawati katika shule inayotarajiwa kujengwa wilayani humo.