Hapo jana Helikopta mmoja ilipoteza mwelekeo na kuanguka katika mto Hudson mjini New York na kumjeruhi rubani ambaye aliokolewa akiwa na majeraha madogo tu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Moto ya mjini New York (FDNY), Helikopta hiyo ilishindwa kutua kwenye pedi na kuanguka ndani ya maji,vyombo vya habari vya mitaa viliripoti.