Wasanii wakubwa nchini Nigeria, ambao pia ni mapacha Peter na Paul Okoye huenda wakaburuzana mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa Paul ametumia picha ya mwenzie kwenye tangazo la tamasha lake nchini Angola.


Peter na Paul Okoye
Peter ambaye yeye ndiye mlalamikaji, amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul Okoye, kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo la muziki.“Kwahiyo wameamua kutumia picha yangu ili wauze tiketi za show yao huko Angola. Nyie mapromota na uongozi mzima mwanasheria wangu atalifuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo,” ameandika Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, tayari Paul Okoye ameshafanya show yake jana Jumapili Mei 26, 2019 usiku nchini Angola.

Peter na Paul ni mapacha na zamani waliunda kundi la P-Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo kadha wa kadha ikiwemo Personally, Temptation na nyinginezo.

Kwasasa kundi hilo limevunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo za maslahi binafasi na kifamilia, Ingawaje kumekuwa na masuluhisho kadhaa ya kurudisha kundi hilo.