Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametangaza kanuni mpya zinazowataka mapadri wote, watawa na viongozi wengine wa kanisa hilo kuripoti matukio ya unyanyasaji wa watoto kingono au kufichwa kwa wakuu wa kanisa hilo kuhusu makosa ya namna hiyo lakini si mamlaka za kiraia.

Papa amefafanua kwamba taarifa za matukio hayo yaripotiwe kwa maaskofu wa mitaa. Lakini ikiwa mtuhumiwa huyo ni Askofu, Kardinali au kiongozi mwingine wa ngazi za juu kanisani, basi makao makuu Vatican yanapaswa kujulishwa.

Kanuni hizo zilizotangazwa juzi zinatarajiwa kuanza kutekelezwa Juni mosi mwaka huu.