Mshambuliaji wa klabu ya Simba na kipenzi cha mashabiki wa miamba hiyo ya soka ya Tanzania, Emmanuel Okwi amewaaga wapenzi wa soka wa Tanzania na kuonyesha nia yake ya kuondoka.Okwi ambaye amekuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Simba ameandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki wake kwa kuandika ujumbe wa ‘good bye’ huku akiwa amehusishwa kutaka kujiunga na klabu kadhaa katika bara hili la Afrika.Mara kadhaa Emmenuel Okwi ambaye ni raia wa Uganda amekuwa akihusishwa na kutakiwa na klabu mbalimbali ikiwemo Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.