NYIMBO za mwanamuziki wa Marekani Drake zimepigwa marufuku kuchezwa kwenye vituo vya radio mjini Milwaukee kwenye kipindi hiki cha fainali ya michezo ya NBA.

Wamiliki wa kituo cha radio KISS-FM kilichopo mjini Milwaukee na Toronto wanasema kupiga nyimbo za drake kwenye kituo chao cha radio ni kuzidi kumpa nguvu kwani yeye atakuwa akipiga domo mwanzo mwisho kuipa nguvu Toronto Raptors kwenye michezo 6 iliyobaki.

Kwenye michezo iyo ya NBA inayoendelea leo alfajiri Timu ya Bucks wameshinda kwa points 108-100.