Mmiliki wa klabu ya Newcastle United, Mike Ashley ameripotiwa kufikia makubaliano ya kuiuza timu hiyo kwa mpwa wa mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour kwa dau la pauni milioni 350.



The Sun imeripoti kuwa mmiliki huyo mpya anayetarajiwa kuichukua wa St James’ Park anayejulikana kwa jina la Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan.

Sheikh Khaled mwenye umri wa miaka 61 ni miongoni mwa wanafamilia ya kifalme kutoka Abu Dhabi ambapo mwaka uliyopita alishindwa kuinunua Liverpool baada ya kutakiwa kutoa dau la pauni bilioni mbili (2bilioni).



Mara kadhaa amekuwa akisema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa mchezo wa soka hasa la Premier League, huku akionekana kutaka kuingia katika listi ya matajiri wakubwa wanao miliki klabu za nchini Uingereza.

Taarifa zinaeleza kuwa tayari mkataba baina ya Ashley na Sheikh umeshasainiwa kwaajili ya kuichukua klabu hiyo kwa pauni milioni 350 na tayari umeshafikishwa kwa wanaohusika na Premier League.

Mpaka sasa klabu ya Newcastle haijatoa taarifa rasmi lakini  The Chronicle imeripoti imethibitisha Sheikh Khaled kuichukua timu hiyo