Mwimbaji kutokea kwenye tasnia ya Bongo Fleva Ommy Dimpoz ameamua kumshukuru Mungu kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kupitia changamoto katika afya yake miezi kadhaa iliyopita hadi kufikia kufanyiwa operesheni ya koo nchini Afrika Kusini.

Ommy Dimpoz ambaye alitoa ngoma ya ‘Ni Wewe’ kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutokana na maajabu aliyomfanyia hadi kupona, tetesi tofautitofauti zilisambaa kuhusu ugonjwa wake na wengi kuzusha kuwa amefariki n.k, ila kupitia ukurasa wake wa instagram ameuliza “Bado najiuliza ni mimi kweli?”

“Nina kila Sababu Ya Kumshukuru Muumba Wetu kwa Pumzi ya Bure, Bado najiuliza Ni mimi kweli?ALHAMDULILAAH 🙏❤️ R.I.P Mzee wangu Dr. Mengi” >>>Ommy Dimpoz