Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amezungumzia namna anavyouchukulia ubingwa wa wapinzani wake Simba ambao wameutangaza jana kwenye mchezo dhidi ya Singida United katika uwanja wa Namfua.

Akizungumza na http://bit.ly/2HvQQZh, Zahera amesema kuwa ubingwa huo haukustahili kuchukuliwa na Simba msimu huu kwa kuwa wamebebwa kwa namna nyingi, jambo ambalo wadau wote wa soka wanalifahamu.

"Ukiniuliza mimi nasema Simba hawakustahili kushinda ubingwa, mambo mengi wamefanyiwa 'fair' na hata wenyewe wanajua na watu wa mpira wanajua", amesema Zahera.

"Mechi nyingi wamebebwa, hata wachezaji wao wenyewe wanakiri suala hilo", ameongeza.

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu hii leo dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Uhuru, Zahera amesema atakosa huduma ya wachezaji wake 6 ambao wanaugua malaria.

"Maandalizi ya mchezo wa kesho (leo) ni kwamba sitokuwa na wachezaji 6 ambao wote ni wagonjwa, nashindwa kuelewa lakini maandalizi mengine yako vizuri kwa mchezo".