Mrembo Lizzy ambaye ni 'Video Vixen wa video mbalimbali za Bongofleva, ameweka wazi kuwa ana ujauzito wa msanii Msami Baby, lakini amempotezea na hapokei simu zake.


Akiongea na eNewz ya East Africa Television, Lizzy amesema kuwa walianza kutofautiana na Msami kwenye kutengeneza Video ya Msami baada ya kulazimishwa kucheza wakati ana ujauzito huo.

''Nina ujauzito wake anatakiwa tu kujua hilo na hii ni baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne, lakini kwasasa hapokei simu zangu na kama ataendelea nitaenda kwa mama yake Mbagala'', amesema Lizzy.

Lizzy amefunguka zaidi kwa kusema anajiamini yeye ndio mke wa Msami na yeye pia anatakiwa kuliheshimu hilo na kuheshimu ujauzito na mtoto wake.

Zaidi mtazame hapo chini akifunguka.