MTOTO wa mwanamuziki R.Kelly , Joann Lee,  ameripotiwa kufukuzwa chuoni kutokana na kutolipa ada. Mtoto huyo ambaye anasoma chuo cha sanaa huko  California, Marekani,  alijikuta anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada kwa wakati baada ya kufika na kutoruhusiwa kuingia.

Meneja wa R.Kelly, Darrell Johnson ametoa taarifa kuwa msanii huyo hakushindwa kulipa fedha hizo ila amesimamisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa za Joann Lee kuacha chuo mwaka 2018. R. Kelly yupo tayari kulipa lakini mpaka atakapoonyeshwa kweli pesa zinahitajika kupitia mfumo wa taarifa maalum (bill statements).

Inasemekana kuwa Kelly na binti yake huyo hawana maelewano mazuri kutokana na Kelly kumlaumu mama wa mtoto huyo akidai kuwa anampandikiza chuki binti yake.