Facebook imeondosha mamia ya akaunti za mitandao ya kijamii na kupiga marufuku kampuni ya Israel kutokana na inachotaja kuwa “Tabia za uongoz zilizoratibiwa” zinazoilenga Afrika. Akaunti hizo bandia mara nyingi huweka taarifa za kisiasa, ikiwemo uchaguzi katika baadhi ya mataifa , kampuni hiyo imesema.Kwa mujibu wa BBC. Facebook imekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kudhibiti taarifa za uongo katika jukwaa hilo la mtandao wa kijamii.

Ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baadaya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani .

Katika ujumbe kwenye blogu, Facebook imesema imeondosha akaunti 265 za mtandao wa kijamii zilizofunguliwa nchini Israel na zilizoilenga Nigeria, Senegal, Togo, Angola, Niger na Tunisia, pamoja na kushuhudiwa “sehemu ya shughuli zake” Amerika kusini na Kuisni mashariki mwa Asia.

“Watu wanaohusika na mtandao huuwalitumia akaunti bandia kuendehsa kurasa hizo, kusabaza taarifa zao na kuongeza mawasiliano kwa njia za uongo.

“Walijifanya kuwa watu kutoka mataifa hayo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari nchini, na kuchapisha na kutuhumiwa kufichua taarifa kuhusu wanasiasa” Nathaniel Gleicher, mkuu a kitengo cha kupambana uhalifu wa mtandaoni katika Facebook, ameandika katika ujumbe huo