Kwa mara ya kwanza wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) wamebaki ndani ya ukumbi wa Bunge wakati zoezi la kuapishwa kwa mbunge mpya wa Arumeru Mashariki (CCM), Dkt. John Pallangyo.



Imekuwa ni kawaida ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi huo wakati wabunge wa CCM wanapoapishwa hasa wale ambao wametoka upinzani na kujiunga na chama tawala.



Jimbo hilo la Arumeru Mashariki lilikuwa likishikiliwa na Mbunge wa Chadema, Joshua Nassari, kabla ya Spika kumvua ubunge wake na kutangaza kuwa jimbo hilo liko wazi ambapo uchaguzi ukafanyika na Dkt John Pallangiyo akaibuka mshindi.