BEKI mwenye mapenzi na Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa bao la kujifunga katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa juzi Ijumaa katika Uwanja wa Uhuru.Simba imejikuta ikipoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa bao hilo na kubakia na pointi zake 81.

Tshabalala alijifunga mwenyewe katika mchezo huo akiwa katika harakati za kuokoa mpira kitendo ambacho kimemfanya awaombe radhi mashabiki wa timu hiyo.Tshabalala alisema kuwa; “Mniwie radhi kwa kilichotokea, najua kuwa nimeigharimu timu yangu lakini makosa ni sehemu mojawapo ya maisha ya mwanadamu, tumepabana sana lakini mwenyezi Mungu hakupenda tupate pointi tatu.”“Kilichotokea hatupaswi kukata tamaa kwani kujikwaa sio kuanguka bado tuna nafasi ya kupambanana kutetea ubingwa wetu,” alisema mchezaji huyo anayeendesha gari aina ya Toyota Raum New Model.