MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji, ametoa usafiri kwa wachezaji wote wa Simba msimu huu ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwao kutokana na mafanikio waliyopata msimu huu.Akiongea leo baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya pili mfululizo, Mo Dewji amesema anatekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wachezaji wa Simba wanakuwa na maisha bora kwa kuwapa pikipiki aina ya Boxer zitakazowasaidia kuongeza kipato.”Kalbu yetu msimu huu imetoa bonus kubwa sana kwa wachezaji ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni moja, na mimi binafsi nimetoa pikipiki kwa kila mchezaji, ambazo zitawasaidia kuinua vipato vyao kwani wakiweka watu wa kuziendesha zinaweza kuwaingizia 15,000/= kwa siku” – Mo Dewji.Aidha Mwekezaji huyo wa Simba amesema kuhusu Pre season ya msimu ujao, wamejipanga kwenda Marekani au Ureno.

”Nimeongea na viongozi wa DC United ya Marekani na nimeomba tukafanye Pre season huko pia tucheze nao na timu nyingine za LMS au kwenda Ureno tukacheze na timu za huko”, ameeleza.Kwa upande wa usajili amesema wapo makini na leo watapata ripoti ya kocha juu ya wachezaji wa nyumbani anaowataka, lakini pia katika wachezaji 10 wa kigeni mpaka leo usiku kocha ataeleza anabaki na nani na kina nani waondoke.