Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine
Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine 
NA FREDY MGUNDA,ILEJE

MKURUGENZI wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi ameshiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje baada ya kupokea kisai cha shilingi bilioni 1.5 kutoka serikalini ili kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwenye ubora unaotakiwa na wananchi wanapata huduma bora za kiafya.

Akizungumza wakati wa ujenzi huo Mnasi alisema kuwa lengo la kushiriki ujenzi huo ni kuhakikisha anaweka hamasa kwa mafundi na wananchi kusimamia vilivyo kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa na serikali kuu.

“Mimi kama kiongozi lazima niwe mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa vitendo hivyo kuja kwangu kushiriki ujenzi huu ni kuonyesha jinsi gani tunatakiwa kufanya kazi tuliyoagizwa na Rais wetu” alisema Mnasi.

Mnasi alisema kuwa atahakikisha bega kwa bega katika usimamizi na ushiriki wa karibu kuhakikisha ujenzi unakamilika na thamani ya fedha(value for money) kwa wakati ili kutimiza malengo ya serikali yanayokusudiwa.

“Nikija mara kwa mara kuangalia ujenzi huu nitahakikisha ujenzi ulio bora wa kuzingatia ujenzi unaofaata hatua zote za msingi na kupata majengo yaliyobora ya hospitali hii ya wilaya” alisema Mnasi

Lakini pia mkurugenzi Haji Mnasi aliishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi kwa kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya.