MGANGA Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi,  amesema kuanzia Januari hadi Mei 2019, watu 1,901 wamepimwa na kuthibitika kuwa wana homa ya Dengue, miongoni mwao, 1,809 wanatoka jijini Dar es Salaam, Tanga 89,  ambapo mikoa ya Singida, Kilimanjaro na Pwani kila mmoja una mgonjwa mmoja.



Amesema hayo leo Alhamisi, Mei 16, 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa wagonjwa ikoani Singida, Kilimanjaro na Pwani wote walitokea Mkoa wa Dar es Salaam na waligunduliwa na ugonjwa huo baada ya kufika kwenye mikoa hiyo.



Aidha, hakuna vifo zaidi vilivyoripotiwa sasa mbali na viwili vilivyoripotiwa awali mwezi huu wa Mei huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari na endapo wataona dalili zilizoainishwa kuhusu ugonjwa huo, wawahi katika vituo vya afya kwa vipimo na matibabu.