Mfanyakazi wa ndani mjini Ryadhi nchini Saudi Arabia amenusurika kifo baada ya kufungwa kwenye mti uliokuwa juani na bosi wake kwa kosa la kuacha samani za ndani juani.

Mwanadada huyo aitwaye Acosta Baruelo, 26 ambaye ni raia wa Ufilipino amesema alifungwa kwenye mti baada ya kuacha baadhi ya samani za thamani juani.

Akielezea jinsi alivyonusurika kwenye adhabu hiyo ya kinyama, amedai kuwa alimuomba mfanyakazi mwenzie wa kike ampige picha kisha asambaze kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya mkononi.

Baada ya tukio hilo, picha hiyo ilianza kusambaa hadi kufikia Mei 9, 2019 tayari Jeshi la Polisi mjini Ryadh lilikuwa limeshaipata nyumba hiyo na kumuokoa mfanyakazi huyo.

Mama huyo aliyetekeleza adhabu hiyo, tayari ameshafunguliwa kesi ingawaje mtuhumiwa wake amesharudishwa nyumbani.

Kufuatia tukio hilo, Ubalozi wa Ufilipino nchini Saudi Arabia ulilazimika kumsafirisha mwanamke huyo kumrudisha nyumbani siku hiyo hiyo aliyookolewa na polisi.