Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa rapper Meek Mill alizuiliwa kuingia kwenye hoteli ya Cosmopolitan mjini Las Vegas huku akidai kuwa sababu kubwa ni ubaguzi wa rangi uliotawala neo hilo, kupitia video ilioachiwa kupitia mtandao wa Instagram imeonyesha Meek Mill akibishana na walinzi hao.

Inaelezwa kuwa rapper huyo alikwenda kwa nia ya kuhudhuria tamasha la Dj Mustard lakini walinzi hao walionekana kumzuia Meek Mill huku wakiwa wametaja sababu kuwa hakufata utaratibu uliowekwa kwenye hoteli hiyo na kudai kuwa lazima wamkamate, hivyo Meek Mill ameichukulia hiyo kama ubaguzi kutokana na asilimia kubwa ya watu weusi kukataliwa kuingia kwenye hoteli hiyo.Inaripotiwa kuwa Mwanasheria wa rapper huyo, Joe Tacopina ameandika barua ikiwataka wamiliki wa hotel hiyo kuomba radhi kwa kitendo hicho ikiwa imeelezwa kuwa ni tabia ya hoteli hiyo kuwazuzia mastaa weusi kuingia mahali hapo

“Hoteli ya Cosmopolitan imekuwa ikifanya muendelezo wa ubaguzi wa rangi na kuzuia mastaa wa rangi nyeusi na watu wengine wa kawaida, wanasema watanifunga najuliza kwa lipi nilishawahi kuwa kwenye sherehe na Jay Z mara moja na wanapenda kuchukua hela zetu, hii inatokea mara nyingi kwa mastaa weusi sio mimi peke yangu, najihisi mjinga baada ya kuwekwa nje na hawa watu weupe bila sababu” >>> aliandika Meek Mill.