Watu wenye silaha wamemuua Kasisi mmoja na Waumini watano wakati wa sala ya Jumapili baada ya kushambulia Kanisa Katoliki kwenye mji wa Dablo, Kaskazini mwa nchi hiyo.


Kwa mujibu wa CNN. Vyanzo vya Usalama na Maafisa kwenye mji huo walieleza kwamba Washambuliaji wapatao 20 hadi 30, waliwasha moto jengo la Kanisa pamoja na majengo mengine jirani na hapo ikiwemo kituo cha huduma za afya,
Shambulio hilo limetokea siku mbili baada ya Wanajeshi wa kikosi maalumu cha Ufaransa kuwaokoa mateka wanne raia wa kigeni huko Kaskazini mwa nchi hiyo katika tukio ambalo Wanajeshi wawili walifariki.


Wanajeshi zaidi kutoka Barsalogho umbali wa Kilometa 45 Kusini mwa Dablo walipelekwa na kuanza msako mara moja juu ya tukio hilo ikiwa ni shambulizi la tatu katika muda wa wiki chache zilizopita dhidi ya makanisa