Mbunge wa Ndanda (CHADEMA), Cecil Mwambe amesema yupo tayari kuwasilisha ushahidi Bungeni kuwa Naibu Waziri wa Viwanda, Mhandisi Stella Manyanya amehusika katika vitendo vya kuomba rushwa.

Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amemtaka Mbunge huyo kuwasilisha ushahidi bungeni Jumatatu 20/5/2019 .

Awali Naibu Waziri wa Viwanda, Mhandisi Stella Manyanya alisimama kuomba mwongozo wa Spika kuhusu tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mbunge Cecil Mwambe, ambapo Naibu Waziri Manyanya alieleza kuwa kama kweli ikithibitika amehusika na vitendo vya rushwa yupo tayari kuwajibika