Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali imejipanga kutoa  huduma zote za afya ikiwemo kununua mashine za kufulia katika Jijini la Dar es salaam.

Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Kisangi (CCM) kuhoji  Serikali ina mpango gani wa kupeleka  mashine za kufulia nguo katika Hospitali za Dar es salaam.

“Tumejipanga kuboresha huduma zote na kununua mashine na madaktari bingwa naomba nilichukue tutatoa majibu ni lini ila tumeanza kuagiza,” amesema Ummy Mwalimu.