Mbatia Alivyopokelewa kwa Shangwe na Wanafunzi Waliounguliwa Mabweni wa Ashira
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia amesema anakusudia kupaza sauti juu ya kuanzishwa kwa somo linalohusu kujiandaa na Majanga “ Disaster Preparedness” katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo ili kuwaandaa wanafunzi kuweza kukabiliana na majanga pindi yanapotokea.

Kauli ya Mbatia ambaye pia ni mtaalamu wa Majanga inakuja siku chache baada ya Mabweni mawili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira iliyopo Marangu Mkoani Kilimanjaro kuungua moto na kuteketeza vitu mbalimbali yakiwemo magodoro, shuka na nguo za Wanafunzi.

Tayari wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa msaada wa kibinadamu kwa Wanafunzi 73 , waathirika wa ajali hiyo ya moto miongoni mwao ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia aliyekabidhi msaada wa mabegi 73 kwa ajili ya kuhifadhi nguo za wanafunzi hao.