Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuanguka kwa chama chake cha Conservative katika uchaguzi wa bunge la Umoja wa Ulaya kunaonesha haja ya bunge kuupitisha mpango wake wa Brexit na kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Chama cha May kimeshika nafasi ya tano baada ya kupata chini ya asilimia 10 ya kura. Chama cha Brexit, ambacho kinaunga mkono Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya bila ya kufikiwa makubaliano kimeshika nafasi ya kwanza.

May ambaye atajiuzulu kuwa kiongozi wa chama cha Conservative mwezi Juni, amesema jana ulikuwa usiku wa kukatisha tamaa kwa chama chake.

Matokeo hayo yanawaunga mkono wale wanaotaka uingereza iondoke katika Umoja wa Ulaya bila ya kufikiwa makubaliano kuhusu jinsi ya kujiondoa pamoja na uhusiano wa Uingereza na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit.