Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 24, 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa ikiwemo kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akieleza hatua zilizofikiwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na nishati ya umeme katika maeneo yote ya Vijijini na mijini ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo akiwemo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bi. Magreth Ikongo (wapili kutoka kulia) hayo yamejiri Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala na Naibu wake Mhe. Costantine Kanyasu (kulia) wakifuatilia hoja za wabunge leo Bungeni wakati wakichangia hoja ya bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, Bungeni jijini Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)