Huenda urusi inakiuka mkataba wa nuklia kwa kufanya majaribio ya silaha za nuklia zisizo na nguvu kubwa katika eneno la Arctic, Afisa wa juu wa intelijensia wa Marekani ameeleza.

Luteni Jenerali Robert Ashley, Mkurugenzi wa taasisi ya intelijensia ya Marekani, amesema Moscow ''pengine inakiuka '' sheria za mkataba.

Alikua akimaanisha mkataba wa pamoja wa Comprehensive Test Ban Treaty (CTBT) unaozuia majaribio ya nuklia.

Urusi, ambayo ilitia saini mwaka 2008, inasema inaunga mkono mkataba wa CTBT.

Marekani imetia saini lakini haijaanza kutekeleza mkataba huo.


Putin na Kim Jong-un waahidi kuimarisha mahusiano

''kwa uelewa wetu uendelezwaji wa silaha za nuklia unatusababisha tuamini kuwa shughuli za majaribio ya Urusi zitasaidia kuboresha uwezo wa silaha za nuklia,'' alisema Luteni Jenerali Ashley.

Ameongeza kuwa Marekani ilitegemea Urusi, ambayo amesema ilikua inategemewa kujaribu silaha zake katika visiwa vya Zemlya, ili kuongeza ubora wa silaha za nuklia kwa kipindi cha muongo mmoja ujao.

Lakini wachambuzi wa mambo wamepokea taarifa hiyo ambayo hata hivyo haikuwashawishi. Shirika linalosimamia utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa nuklia CTBTO imesema kwenye taarifa yake kuwa haishuku shughuli zozote zinazokwenda kinyume na mkataba.

CTBT, ambao inapiga marufuku majaribio ya silaha za nuklia popote pale duniani, ulifikiwa na Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa mwaka 1996.