Mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation, Tony Elumelu, akiwa katika moja ya mikutano ya wajasiriamali wa Afrika nchini Nigeria.
Washiriki wa moja ya mikutano iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja na mwasisi wa Tony Elumelu Foundation.

*Kukutanisha wajasiriamali 5,000 wa Bara la Afrika

Na MWANDISHI WETU -Abuja, Nigeria.

Taasisi ya Tony Elumelu Foundation (TEF) ambayo inapambania wajasiriamali kutoka Afrika itakuwa mwenyeji wa awamu ya 5 ya mkusanyiko mkubwa wa wajasiriamali kutoka Afrika itakayofanyika Julai 26 na 27, 2019, ambapo mkutano huo wa siku mbili utafanyika Hoteli ya Transcorp Hilton, Abuja nchini Nigeria.

Mkutano huo wa kila mwaka huandaliwa kupitia Programu ya Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship ambayo imewapa mafunzo Waafrika chipukizi 3,000 ambao walichaguliwa kutoka zaidi ya waombaji 216,000.

Tukio hilo linawapa nafasi wanawake na wanaume chipukizi kutoka nchi zote 54 za Afrika kukutana, kujifunza na kubadilishana mawazo yenye mlengo wa kuwa wawekezaji bora Afrika na duniani.

Pia ni fursa muhimu kwa viongozi wanasiasa na watunga sera kukutana uso kwa uso na kizazi kipya cha wafanyabiashara viongozi Wafrika ambao wanabadilisha uchumi wa Afrika.

Wazungumzaji wakuu katika warsga hiyo muhimu ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na Rais wa Senegal, Macky Sall, ambao wataungana na Mwanzilishi wa TEF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Heirs Holdings na United Bank for Africa (UBA), Tony O. Elumelu, katika majadiliano ya wazi.

Uwepo wa marais hao unawapa fursa wajasiriamali kutoka Afrika wanaohudhuria kuwa na mjadala wa kina na kutoa ushuhuda namna serikali inavyoweza kufanya kuchochea ukuwaji wa biashara.

Ajenda ya mkutano huo inahusisha majadiliano na wataalamu kutoka Afrika na duniani ambao watawapa mafunzo washiriki kuongeza ujuzi katika biashara yao. Aidha warsha hiyo itawapa fursa baadhi wajasiriamali wateuli kuelezea bidhaa na huduma wanazotoa mbele ya jopo la majaji.

Kwa mara ya kwanza, warsha hiyo itafanyika Abuja, Nigeria na kuwaleta pamoja watunga sera wakubwa, wafanyabiashara wakubwa na wale waliowahi kufaidi Programu hiyo.

Mwaka jana, tukio muhimu lilikuwa uzinduzi wa TEFConnect ambayo ni sehemu ya wajasiriamali kutoka Afrika kubadilishana mawazo kupitia mfumo wa digitali.

Mikutano hiyo imewahi kuhudhuriwa na marais kadhaa wakiwamo Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, Waziri Mkuu wa mstaafu wa Benin na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri, Lionel Zinsou na Makamu wa Rais wa Nigeria, Profesa Yemi Osinbajo.

Taasisi ya Tony Elumelu imedhamiria kuleta mabadiliko Afrika nzima kupitia ujasiriamali kwa kutaka zaidi Waafrika kujitegemea, Africapitalism, chini ya mwanzilishi huku akitambua zaidi kuwawezesha vijana wa Afrika kiuchumi hususan karne hii ya 21.

Mwaka 2015, taasisi hiyo ilijitolea dola za Marekani milioni 100 million kuwawezesha wajasiriamali 10,000 kutoka kote barani kwa zaidi ya miaka 10 ambapo kwa sasa inakwenda kutimiza miaka mitano.

Pia Tony Elumelu Foundation imetoa mchango wa kushauri na kutoka mafunzo ya menejementi kwa zaidi ya watu 7,500 wanaoanzisha na wenye biashara ndogo kwa nchi zote 54 za Afrika.

“Warsha ya TEF Entrepreneurship haitaleta tu watu wadau muhimu katika mabadiliko ya ujasiriamali wa Afrika lakini pia kumpa nafasi kila mtu kupanua biashara yake kwa nia ya kuleta maendeleo barani.

“Tunafarijika kupokea habari kutoka kwa wajasiriamali wetu ambao wanatengeneza ajira, wanaajiri watu na kubadilisha maisha ya jamii inayowazunguka barani Afrika. Tunaamini hawa wajasiriamali ni tegemeo wetu wa baadaye. Wekezeni kwao sasa na kuvuna ndoto ya kesho ya Afrika,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TEF.Ifeyinwa Ugochukwu.