Baada ya Afande Sele kumshambulia kwa maneno makali msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kwa kusema kuwa ni mshamba na hana elimu ya kuiongoza klabu hiyo kwani ameunga unga tu elimu ya darasani . Hatimaye Haji Manara amejibu mashambulizi hayo kwa kusema hamjui msanii huyo na hata nyimbo zake hazijui.