VIDEO Queen na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Irene Louis amefunguka kuhusu picha yake inayosambaa mitandaoni, ambayo inamwonyesha ameharibika sana usoni hali iliyosababisha mashabiki kuhoji kulikoni.  Akizungumza na MIKITO mrembo huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Chomeka alichomshirikisha msanii mwenzake Shetta, Lynn amewaka akisema hataki kusikia habari hizo kabisa.

“Jamani hebu niacheni kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya, sijui kwa nini watu wanapenda kufuatilia mambo yasiyo na maana, wanaacha kufuatilia mambo muhimu, wanahangaika na mimi. “Jamani nisapotini kwenye muziki wangu inatosha, lakini kutwa mmekaa mnauliza nini kimenikuta usoni, sasa hata nikiwaambia nyie itawasaidia nini? Mnachosha bwana,” alisema mrembo huyo kwa hasira.