Kodak Black Anyimwa Dhamana, Arudi jela Kutumikia Kifungo Chake
Inaripotiwa kuwa Rapper Kodak Black amenyimwa dhamana kutokana na kesi yake ya kumiliki silaha kinyume cha sheria ambapo pia alidaiwa kusababisha maafa kwenye U.S. Marshals na silaha hizo.

Inaelezwa kuwa Jumatano ya May 29,2019  Kodak Black alifikishwa Mahakamani na Jaji Mkuu aliamua kutoa maamuzi kuhusu kesi hiyo na kuelezwa kuwa Kodak atabaki akitumikia kifungo chake cha miaka 10 gerezani mpaka pale kesi yake itakaposikilizwa tena mwezi September mwaka huu.

Hata hivyo May 21,2019 Kodak alifunguliwa shtaka lingine akiwa gerezani baada ya Promota Nicholas Fitts kudai kuwa alishindwa kutumbuiza kwenye matamasha aliyopangiwa kwa mara kadhaa na kuvunja makubaliano aliyokuwa ameyaweka ndani ya mkataba.