Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amemwambia nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Ibrahim Ajibu kufikilia mara mbili kuhusu kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Imeelezwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zahera amedai Ajibu ni kiongozi wa wenzake na hapaswi kuwa na mawazo ya kuondoka Yanga na kuwaacha wenzake.

Mkataba wa Ajibu na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu na inadaiwa kuwa atajiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kuisha na Yanga.

Taarifa za Ajibu kuondoka Yanga zimeanza muda mrefu uliopita na kuleta sintofahamu kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na namna mwenendo wa klabu ulivyo.

Zahera amemuomba Ajibu afikirie zaidi ya mara moja kuhusiana na kuondoka kwake kwa manufaa ya Yanga maana anaheshimu mchango wake.