Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha AICC Chaingiza Mapato Zaidi Ya Shilingi Bilioni 11
Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha hotuba ya mpango na Makadirio ya Bajeti ya wizara kwa mwaka  wa fedha  2019/2020 ,  bungeni jijini Dodoma  ambapo kituo cha kimataifa cha mikutano  Arusha  AICC  kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia  ya mikutano hapa nchini na kuchangia katika uchumi wa taifa.

Akiwasilisha hotuba  ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mei 30, 2019 bungeni jijini Dodoma  ,Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi amesema hadi kufikia Mwezi April ,2019  kituo cha mikutano ya kimataifa cha Arusha AICC  Kimeingiza  mapato ya Sh.Bil.11,Mil.428  laki 8  ,68 elfu na mia 998.

Kati ya Fedha hizo,Sh.Bilioni 2 ,Mil.76,laki 7 ,71 elfu na 27[2,076,771,027] zimetokana na huduma  za mikutano 342  iliyofanyika katika kituo cha AICC  ambapo mikutano 32 kati ya hiyo ni ya kimataifa na 310 ni ya kitaifa.

Prof.Kabudi amefafanua kuwa ,Sh.Bilioni 2,Milioni 244 , laki 5,na 32 elfu  na mia 662 [2,244,532,662] zimetokana na huduma za mikutano  katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere ,Sh.Bil.3,mil 556,laki 5  na 96 elfu na mia 819[3,556,596,819] na Sh.bil.3,mil.550,laki 9,na 68 na mia 490 [3,550,968,490]ni kutokana na huduma za hospitali.

Aidha,Prof.Kabudi amesema ,kuhusu usimamizi wa kiuchumi Ripoti inaonesha kuwa Tanzania imeendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo ikiwianishwa na mpango wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa [2030] na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika,Mpango wa Miaka mitano[FYDP  II 2016/17-2020/21] unaweka mkazo katika mageuzi ya viwanda na maendeleo ya Rasilimali watu kama njia sahihi ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

Hata hivyo,Successor Strategy ya Zanzibar 2016/17-2020/21 imepatia ufumbuzi  maeneo mengi yaliyokuwa yameainishwa   kama mapungufu  kama mpango kazi wa  APRM.

Katika hatua,nyingine Prof.Kabudi katika hotuba yake amesema chuo cha Diplomasia kimeendelea kutoa mafunzo  na kufanya tafiti katika masuala ya Diplomasia ,uhusiano wa kimataifa na usuluhishi wa Migogoro na kulinda Amani.

Chuo cha Diplomasia kinatoa Mafunzo ya Lugha saba [7] za kigeni  ambazo ni kiarabu,kichina,Kifaransa,kiingereza,Kireno,Kihispania,na Kikorea na hadi sasa kinafanya Mazungumzo na Serikali ya Kirusi  ili kufadhili mafunzo ya Lugha ya Kirusi na Mwaka 2018/2019 kilidahili Jumla ya wanafunzi  1,029  katika ngazi za cheti,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili.