KIPA wa Simba anayeichezea Ndanda FC kwa mkopo, Said Mohamed ‘Nduda’ amesema yupo tayari kuitumikia Yanga msimu ujao.Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni mara baada ya aliyekuwa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kusitisha mkataba wa kuichezea timu hiyo na kuwa huru kusaini popote.Kipa huyo, hivi sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuichezea timu nyingine itakayomhitaji kwa mujibu wa kanuni za soka kwa kuwa mkataba wake umesaliwa na mwezi mmoja pekee.Akizungumza na Championi Ijumaa, Nduda alisema yupo kuichezea Yanga kama wakihitaji huduma yake. “Ujue mimi soka ni kazi ambayo inaendesha maisha yangu ya kila siku, kitu cha kwanza ni maslahi yatakayoniwezesha nisaini mkataba kwenye timu itakayonihitaji kwenye msimu ujao wa ligi.“Yanga ni timu yangu niliyowahi kuichezea, hivyo sitapata tabu kama nitarejea, nitakuwa kama ninarudi nyumbani kwani ni moja ya timu zilizonifikisha hapa nilipo katika maisha yangu ya soka baada ya Majimaji.“Nitasaini mkataba wa kuichezea Yanga kama watakubali kunipa kile ninachokihitaji, kuhusu mipango ya kurejea Simba bado sijajua, mkataba wangu unakwenda ukingoni na hakuna mazungumzo yoyote na mabosi wa Simba,” alisema Nduda.