MWANAMITINDO Mmarekani,  Kim Kardashian,  ameamua kurudi kuisaidia jamii na kuanzisha kampeni yake kusaidia wafungwa iitwayo “90 DAYS OF FREEDOM’’ akishirikiana na wanasheria Brittany K, Barnett na Miangel Cody, kwa kipindi cha miezi mitatu.Kampeni iyo amesaidia kuwatoa jela wafungwa 17 huku baadhi yao akiwasaidia kupata makazi na ajira. Hii ni baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kusaini hatua ya kwanza ya sheria inayoruhusu baadhi ya watu waliofungwa kwa tuhuma za dawa za kulevya kuomba kupunguziwa adhabu.

Kwa kipindi hiki Kim Kardashian amekuwa akipokea simu nyingi kwa watu mbalimbali wakihitaji msaada wa ndugu zao waliopo jela ili wapatiwe msaada wa kuachiwa uhuru