Kim Kardarshian na Kanye West ambaye ni Nyota wa kipindi cha Televisheni cha maisha halisi kinachofaamika kama The Keeping Up with the Kardashians , mwenye umri wa miaka 38, amethibitisha kupitia ukurasa wake waTwitter kwamba yeye na mumewe mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka wamemkaribisha mtoto wao wa kiume wa nne kwa uzazi wa kusaidiwa.

"Yuko hapa na hana kasoro!" Kardashian West alituma ujumbe wa Tweeter.


Kim na Kanye walikuwa na watoto watatu akiwemo mvulana anayeitwa Saint na msichana anayeitwa North
Ilithibitishwa mwezi wa januari kwamba wawili hao wangempokea mtoto wa nne ambaye angejiunga na ndugu zake wakiwemo wasichana Chicago, mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu na North, atakayetimiza umri wa miaka 6 mwezi ujao pamoja na Saint, mwenye umri wa miaka 3.

Taarifa kwamba mtoto huyo wao ambaye angezaliwa kupitia mwanamke mwingine alikuwa katika chumba cha uzazi zilifahamika Alhamisi wiki hii wakati wa kipindi cha The Ellen DeGeneres Show.

Kardarshians Januari 14 , Kardashian West alithibitisha taarifa juu ya ujauzito wa mwanae kupitia mwanamke ambaye hakutajwa jina baada ya kuulizwa iwapo ''anampango wa kumpata mtoto mwingine''

"Ndio tunao," alijibu nyota huyo wa kipindi cha maisha halisi, na kuongeza kuwa mtoto anakaribia kuzaliwa "hivi karibuni ."

"Ni mvulana, Nadhani hili limekuwa likihfahamika ,"alisema Kardashian West. "nililewa wqakati wa sherehe zetu za Christmas na nikawaambia baadhi ya watu. Siwezi kukumbukani nani nilimwambia kwasabababu kwa sijawahi kulewa." Kim hakuelezea ni lini hasa atazaliwa, licha ya kusema atazaliwa hivi karibuni


Awali Kim alisema kuwa kuongezeka kwa uhalifu wa bunduki nchini Marekani kulimfanya 'asite' kupata watoto zaidi wakati alipokuwa akifanya kipindi cha Keeping Up With The Kardashians mwaka 2018.

lakini pia akasema kuwa Kanye alikuwa anataka sana kupata watoto zaidi, akisema kuwa a;limwambia anataka watoto jumla saba.

Kim alionywa na madaktari kuwa asijaribu kupata mtoto mwingine kutokana na matatizo ya kiafya aliyo nayo.