Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Renatus Mchau (kwanza kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Abuu Mussa Mjaka (mwenye suti nyeupe) wakikabidhiana mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya na hospitali kwa Mwanasheria wa kampuni ya Pan African Energy Bi.Rita Mahele (wa pili toka kushoto) pamoja na  Meneja uhusiano wa Pan African Energy Andrew Kashangaki.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Renatus Mchau (kwanza kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Abuu Mussa Mjaka wakisaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya. Anayeshuhudia kushoto ni Mwanasheria wa kampuni ya Pan African Energy Bi.Rita Mahele.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Abuu Mussa Mjaka (kulia) akisaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya na Mwanasheria wa kampuni ya Pan African Energy Bi.Rita Mahele (kushoto).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Abuu Mussa Mjaka akiwakaribisha wajumbe katika kikao cha utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya na Hospitali
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Renatus Mchau akizungumza machache katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya na Hospitali.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dr.Halfanis Melkizemba akieleza machache.

Picha ya pamoja.

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa kati viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa.

Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na halamshauri yake kuweka nguvu katika kuzitatu.

‘Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya ambapo vituo vinne vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika kuendeleza sekta ya Afya.

Alisema msaada huo wa Pan African utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita ambapo kati ya hivyo vituo vinne vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kuongeza damu kwa wanawake wajawazito.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukuru kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha Nangurukuru.

‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka.

Ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga ulianza kwa Mchango wa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta ambapo zaidi ya shilingi milioni sabini kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli wa shiingi milioni ishirini(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017 akiwa katika ziara mkoani Lindi.

Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia nguvu zao.

Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti na chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni mia nane na thelathini.

Katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na Bohari ya dawa thamani ya shilingi milioni mia nne.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo.