Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Mahakama hiyo,  Kelvin Mhina alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa ila upelelezi haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Naye wawili wa utetezi Charles Kisoka alidai kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Hata hivyo baada ya kauli hiyo wakili wa serikali Saimon ameyasikia maombi ya upande wa utetezi hivyo watajitahidi kuwahimiza wenzao kuharakisha upelelezi na wanategemea tarehe nyingine ya kutajwa watatoa mrejesho wa kile Kinachoendelea.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Juni mwaka mwaka huu.

Mmiliki huyo wa blog ya 8020 Fashion na mume wake, alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.