Hadi sasa watu 1901 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Dengue nchini huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ukiwa na wagonjwa 1800, maambukizi yanaelezwa kupanda kwa kasi hadi watu 74 kwa siku kutoka watu 32.
Wameibuka baadhi ya watu wanaodai kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kwa kutumia 'maji ya mpapai', Naibu waziri, Wizara ya Afya, Wazee Jinsia na Watoto, Mh. Faustine Ndugulile amelitolea ufafanuzi; .
''Nataka niwaambie ugonjwa huu hauna tiba iliyothibishwa, wengine wamekuja na tiba ya maji ya mpapai, hakuna tiba sahihi ya kutibu ugonjwa huu"