Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kubatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu, Chama cha CHADEMA kimetoa kauli kuhusu uamuzi huo.

Akizungumza na Ayo Tv na Millardayo.com, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumain Makene amesema uamuzi wa mahakama ni wa Kihistoria kwa kuwaondolea mamlaka Wakurugenzi.

“Uamuzi huu wa Kihistoria na ni changamoto kwa watawala ili kuhakikisha nchi inafanya uchaguzi na kuwa na uchaguzi unaomuhakikishia mpiga kura kumchagua mtu kwa uhuru,“amesema.