KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa aliwaambia wachezaji wake Simba ni timu kubwa ila ni lazima wapate matokeo kwa namna yoyote ile hivyo wanaowasema vibaya watakuwa wanasumbuliwa na wivu.

Kagera Sugar imeipiga Simba nje ndani baada ya mchezo wa kwanza uwanja wa Kaitaba kushinda mabao 2-1 na wa jana uwanja wa Uhuru kushinda kwa bao 1-0 ambalo walizawadiwa na nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa hakuwa na hofu kuikabili Simba kwa kuwa alitambua kuwa kama ipo ipo tu.

"Niliwaambia wachezaji wangu tunakwenda kucheza na timu kubwa, lazima tushinde Mungu yupo pamoja nasi atatupigania twendeni na ikawa hivyo tumeshinda kwa kupewa zawadi ya goli, ni Mungu mwenyewe ametenda.

"Tulianza vibaya msimu huu ila hiyo haikunipa tabu kwa kuwa vijana walikuwa wanacheza sasa kushinda kwetu ni furaha na inaleta heshima kwa wachezaji pia," amesema.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza michezo 35 imejikusanyia pointi 46.