Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kuacha mara moja kuvamia na kuingilia maeneo ya Jeshi ambapo tayari kuna Oparesheni iliyoanza ya kuwaondoa watu katika maeneo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa  JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema kama wananchi wanataka kununua maeneo karibu na Jeshi basi wafanye tathimini ya kuuliza kwa Jeshi kabla ya kununua ili kuepusha migogoro.

Pia amesema maeneo hayo yanaonekana ni ya wazi ama misitu yameachwa kwa malengo maalumu kwani mchana yanaonekana ni Msitu lakini usiku ndio Hoteli za Jeshi kwa sababu wanafanya warsha na makongamano misituni.