Jumla Ya Miradi 88 Ya Maji Nchini Imejengwa Chini Ya Kiwango
Jumla ya Miradi 88 ya Maji hapa nchini imejengwa chini ya     Kiwango kwa  kipindi cha mwaka 2010 na 2015 hali iliyosababisha pawe na kero  kubwa ya uhaba wa maji hususan Maeneo ya vijijini hadi sasa.

Hayo yamesemwa  Mei 29,2019  bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa  wakati akijibu swali  mbunge Wa Moshi Vijijini  Anthony Komu aliyehoji  serikali inafanya mpango gani wa  kubainisha  waliohusika na mapungufu  yaliyobainika   na kuwachukulia hatua.

Katika majibu yake Prof.Mbarawa amesema  kuna miradi 88  ya Maji Tanzania imejengwa chini ya kiwango  kwa mwaka 2010  hadi 2015 na nia ya serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha watanzania wanapata Maji ya Uhakika na kama mradi umejengwa chini ya Kiwango serikali bado inafanya uchunguzi na ikishakamilisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waliohusika.

Katika hatua nyingine Prof.Mbarawa amesema serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi  kwa kushirikiana na mkandarasi wa barabara  wameweza kukarabati  na kumaliza tatizo la uvujaji maji barabarani kwa gharama ya Tsh. Mil.1 laki 4 na 37 elfu[1,437,000/=]