Mkuu  Wilaya ya Kisarawe,  Jokate Mwegelo amesema mitandao ya kijamii ni kama kisu ukiitumia vibaya.

Jokate amewaasa vijana kuwa huenda mitandao hiyo ilifika wakati wengi wakiwa bado hawajajiandaa lakini matumizi sahihi ya nyenzo hiyo yanaweza kuwafikisha mbali kiuchumi.

 "Mitandao ya kijamii ni kama kisu, ukichinja kuku utakula na kufurahi lakini ukikitumia vibaya utamjeruhi mtu na hata kumuua halafu utapata kesi, kwa hiyo mitandao ya kijamii ni nyenzo tukitumia vizuri,"  amesema  Jokate.

"Nimeona dunia ya pili ya mitandao kwa sababu vijana wengi wameunga mkono kampeni hii na inaendelea vizuri," amesema Jokate.

DC Jokate ameyazungumza hayo leo katika mdahalo ulioandaliwa na Plan International  kuhusu namna usawa wa kijinsia unayoweza kuchochea maendeleo.