Kamanda wa vikosi vya Jubaland huko Jamame, Mural Ahmed Farah amewaambia wanahabari kuwa vikosi maalumu vya Somalia, vinavyojulikana kama Danab, na vikosi vya Jubaland vikisaidiwa na washirika wa kimataifa vimewaua magaidi hao baada ya kupokea taarifa kuhusu maficho yao. Ameongeza kuwa sita kati ya waliouawa kwenye operesheni hiyo ni wataalamu wa mabomu.

Oparesheni hiyo ya Jumatano imekuja kabla hata ya kupita siku mbili baada ya vikosi vya Somalia kuwaua magaidi 11 wa al Shabaab kwenye mapigano yaliyotokea mkoa wa Shabelle ya kati kusini mwa Somalia.

Wakati huohuo vikosi vya usalama vya Somalia vimewakamata magaidi  wanne kwenye opresheni iliyofanywa Weydow.

Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakishirikiana na askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wameimarisha vita dhidi ya magaidi wakufurishaji wa al-Shabab katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia ambapo wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi wengi.

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wakufurishaji wa Al Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.