Japan na Urusi Zashutumiana
Mawaziri wa mambo ya nje wa Japan na Urusi waliokutana kwa mazungumzo katika mji mkuu wa Japan, Tokyo, wameshutumiana kwa serikali zao kujipanua kijeshi katika visiwa vya Kurils.

Japan imesema kujipanua kijeshi kwa Urusi katika visiwa hivyo vinavyozozaniwa ni hatua isiyokubalika, huku Urusi ikisema mpango wa Japan wa kuweka mfumo wa kujilinda na makombora uliotengenezwa Marekani kwa jina la Aegis Ashore ni tishio kubwa kwa nchi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Takeshi Iwaya, alimjibu mwenzake wa Urusi Sergei Shoigu kuwa mfumo huo ni wa kujilinda tu, na kamwe haototumiwa kuidhuru Urusi au nchi nyingine yoyote.

Visiwa hivyo vinavyozozaniwa vilikamatwa na Umoja wa Kisovieti kutoka Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia.