Kwa mara ya kwanza Jacqueline Mengi amzungumzia Dkt. Mengi
Tangu kutokea kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP Dkt. Reginald Mengi, mkewe ambaye ni Jacqueline Mengi amekuwa kimya kwenye mitandao ya kijami, sasa leo kwa mara ya kwanza amevunja ukimya huo.

Jacqueline Mengi ambaye alipata kuwa Miss Tanzania mwaka 2000 ametumia mtandao wa kijamii wa Twitter kueleza kuwa leo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Dkt. Mengi.
Kwa mara ya kwanza Jacqueline Mengi amzungumzia Dkt. Mengi


“Leo tungekuwa tuna kusheherekea wewe, kama nikifumba macho yangu naweza kuona namna unavyo tabasamu pale tunapokuimbia heri ya kuzaliwa. Hakuna neno la kuelezea ni kiasi gani Mimi na watoto tulivyokukumbuka, kuamka kila siku bila wewe. Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu wa kweli, milele mioyoni mwetu.” ameeleza.

Marehemu Dkt Reginald Mengi alifariki May 2,2019 akiwa Falme za Kiarabu Dubai kwa ajili ya matibabu na leo hii May 29,2019 angekuwa akitimiza miaka 75.